LAGOS, Nigeria
KWA mujibu wa Kamati ya Amani nchini Nigeria, yamejitoza matukio ya uvunjifu wa amani 109 tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Januari, 2027.
Kampeni zilianza rasmi Agosti 19 na Novemba 15, 2026, kikundi cha wananchi wenye silaha kilivamia msafara wa Gavana wa zamani wa Jimbo la Kano, Rabiu Kwankwaso.
Kwankwaso, ambaye kwa sasa anagombea kiti cha Makamu wa Rais kupitia Chama cha National Democratic Congress, alikuwa akielekea kwenye kampeni zake.
Matukio ya aina hiyo yaliripotiwa pia katika moja ya mikutano ya kampeni ya Makamu wa Rais wa zamani, Atiku Abubakar, akiwa kwenye majimbo ya Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria.
Ni kutokana na mfululizo wa matukio, jumuhiya za kimataifa, likiwamo Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International, zimeonya juu ya mambo kuwa mabaya Zaidi kadiri siku zinavyozidi kusogea kuelekea Uchaguzi.
Kwa upande wake, Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, naye amepaza sauti kulaani kile kinachotokea katika mikutano ya kampeni.
Hata hivyo, kwa Nigeria hii si mara ya kwanza kwa chaguzi zake kuandamwa na matukio ya aina hii. Zitakumbukwa vurugu kubwa zilizojitokeza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2011 na kusababisha vifo vya watu 800.


