21.5 C
New York

Lurhex Production yazidi kutikisa, wasanii wake wang’ara Afrika Mashariki

Published:

Na Christopher Msekena, Gazetini

WASANII wanaounda lebo ya muziki ya Lurhex Production wanaendelea kujizolea umaarufu kupitia kazi zao, huku kampuni hiyo ikiendelea kuimarisha juhudi za kukuza vipaji na kupanua wigo wa wasanii wake katika soko la muziki Afrika Mashariki.

Kwa sasa, lebo hiyo inasimamia wasanii kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao ni Benika Zey, Joelike na Rajul Malik. Kila mmoja kwa nafasi yake anaendelea kujenga jina kupitia kazi za muziki zinazovutia mashabiki katika ukanda huo.

Akizungumzia mwenendo wa lebo hiyo, Meneja wa Lurhex Production, Rodrigue Heri, amesema mashabiki wanapaswa kujiandaa na ujio wa video rasmi ya wimbo wa Monica, ulioimbwa na Benika Zey, ambayo inatarajiwa kutoka Ijumaa hii.

Amesema wimbo huo tayari umeanza kupata mwitikio kwenye mitandao ya kijamii, ambako mashabiki wamekuwa wakishiriki katika changamoto mbalimbali za kucheza muziki huo, hali inayochangia kuongeza umaarufu wake kabla ya video rasmi kutoka.

Kwa upande wake, Joelike anaendelea kujiandaa na ujio wa wimbo wake mpya unaoitwa Niache, ambao kwa mujibu wa Rodrigue, unatarajiwa kupatikana hivi karibuni kupitia mtandao wa TikTok.

“Wasanii wetu wanaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuwafikia mashabiki wengi zaidi na kupanua wigo wa muziki wao katika Afrika Mashariki,” amesema Rodrigue.

Wakati wasanii wenzake wakiendelea na maandalizi ya kazi mpya, Rajul Malik anaendelea kufurahia mafanikio ya wimbo wake Joy, ambao umevuka watazamaji 400,000 kwenye mtandao wa YouTube.

Mafanikio ya wimbo huo yameambatana na ongezeko la maonesho ya muziki, huku msanii huyo akipata mialiko ya kufanya shoo ndani na nje ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Related articles

Recent articles