CATALUNYA, Hispania
KOCHA wa Barcelona, Hansi Flick, ametoa mtazamo wake akidai kuwa kinda wake, Pau Cubarsi, ndiye aliyestahili kutwaa tuzo ya Kopa yam waka huu wa 2026.
Kwa mwaka wa tatu mfululizo, Lamine Yamal alitwaa tuzo hiyo ya Ballon d’Or inayotolewa kwa mchezaji mwenye umri wa chini ya miaka 21 [U-21].
Hata hivyo, wakati anakabidhiwa tuzo hiyo, Yamal mwenye umri wa miaka 21 alikiri kuwa Cubarsi ndiye aliyestahili zaidi.
Kama itakumbukwa, Cubarsi alifanya vizuri wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026, ambapo ndiye aliyeibuka Kinda Bora wa michuano.
Akizungumzia hilo, Flick anayefanya kazi na wachezaji hao katika kikosi cha Barcelona, alisema: “Nilipenda alichokisema Lamine kuhusu Pau Cubarsi. Alistahili tuzo ya Kopa kwa msimu mzuri aliokuwa nao.”


