LONDON, Uingereza
HARRY Kane ndiye aliyeibuka na kicheko mwanzoni mwa wiki hii baada ya kuitwaa ile tuzo maarufu ya soka ya Ballon d’Or kwa mwaka 2026. Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika jijini London, Uingereza.
Straika huyo wa Bayern Munich na timu ya soka ya Taifa ya England alitangazwa mshindi mbele ya Kylian Mbappe [Real Madrid, Ufaransa] na Lamine Yamal [Barcelona, Hispania].
Ni kwa maana hiyo, Kane anakuwa Muingereza wa kwanza kuibeba tangu Michael Owen alipoibeba mwaka 2001 akiwa na kikosi cha Liverpool.
Kwa upande mwingine, bado Barcelona na Real Madrid zinabaki kuwa ndiyo klabu za soka zenye tuzo nyingi za Ballon d’Or, ambapo kila moja imebeba mara 12.
Klabu za Ligi Kuu ya Italia [Serie A], Juventus na AC Milan, zinafuata kila moja ikiwa na tuzo nane, wakati Bayern Munich na nane, huku Manchester United nayo ikiwa imekusanya mara nane .


