LONDON, Uingereza
LEJENDARI wa Manchester United, Paul Scholes, amemshauri kiungo wa timu hiyo, Bruno Fernandes, kuondoka katika soka la Ulaya na kutimkia Ligi Kuu ya Saudi Arabia.
Bruno alikosolewa na kocha Michael Carrick baada ya Man United kutandikwa mabao 4-1 na Como katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita.
Ni kutokana na kiwango chake hicho, Mreno huyo aliachwa benchi kwa dakika zote 90 za mchezo uliofuata dhidi ya Bournemouth.
Taarifa zinaeleza kuwa Carrick na Bruno walikaa mezani na kuzungumza kuelekea mchezo wao wa wikiendi hii dhidi ya Chelsea.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa bado hakuna uhakika wa asilimia 100 kwamba Bruno atakuwa pale Stamford Bridge msimu ujao.


