15.3 C
New York

Tuzo za CAF sasa Desemba 7

Published:

CAIRO, Misri

TUZO za mwaka huu za Shirikisho la Soka barani Afrika [CAF] zitatolewa Desemba 7, 2026 katika hafla itakayofanyika jijini Lagos, Nigeria.

Kama itakumbukwa, hii itakuwa mara ya nne kwa Lagos kuwa mwenyeji wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo baada ya kufanya hivyo mwaka 2008, 2013 na 2014.

Inafahamika kuwa miongoni mwa tuzo zitakazogawiwa siku hiyo ni pamoja na ile ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa CAF.

Kabla ya siku ya tuzo, Nigeria itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa CAF unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Novemba 21, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CAF, Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bola Ahmed Tinubu [BTICC] mjini Abuja.

Related articles

Recent articles