LONDON, Uingereza
BEKI wa timu ya Taifa ya Argentina, Cristian Romero, amefichua kuwa Lionel Messi ndiye aliyempendekeza kupewa kitambaa cha unahodha wa kikosi hicho.
Romero ameyasema hayo katika mahojiano yake idara ya mawasiliano ya kampuni ya vifa vya michezo ya Adidas. “Alinichagua kuwa nahodha na ni jambo zuri sana …” amesema.
Kwa upande mwingine, nyota mwingine wa Argentina, Lisandro Martinez, amemsifia Messi akisema staa huyo aliifanya timu hiyo kuwa na Umoja.
“Leo hakuwaunganisha wachezaji pekee, bali taifa zima kwa ujumla. Huu ni mfano mzuri wa heshima kubwa aliyoiacha kikosini,” anmesema Martinez anayekipiga Manchester United.
Messi alishastangaza uamuzi wa kustaafu kuitumikia timu ya taifa lakini zipo taarifa kuwa atacheza mechi ya mwisho hivi karibuni.


