LONDON, Uingereza
KIUNGO wa zamani wa Chelsea, Craig Burley, amemtaka Cristiano Ronaldo kukubaliana na ukweli, kwamba kwa sasa si mchezaji muhimu kwenye kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Ureno.
Ronaldo aliondoka kwa hasira kwenye kambi ya Ureno wakati timu hiyo ikijiandaa kuikabili Denmark katika mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya [UEFA Nations League].
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 41, aliodoka baada ya kugundua kuwa hakuwa sehemu ya kikosi kilichokuwa kimepangwa na kocha Jorge Jesus.
Kwa upane wake, Burley ameunga mkono uamuzi wa Jesus kutokumpa nafasi Ronaldo, akisema staa huyo hapaswi kuwa straika tegemeo kwa umri wake wa miaka 41.
“[Ronaldo] bado anajiona ni muhimu, anajiona mkubwa lakini haiko hivyo tena. Huyu siye Ronado wa umri wa miaka 28, siye Ronaldo wa miaka 25 wala 32. Ana umri Zaidi ya miaka 40 …” amesema.
Bila uwepo wa Ronaldo, Ureno ilipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Denmark, wafungaji wake wakiwa ni Joao Cancelo, Goncalo Ramos, Vitinha na Joao Felix.


