MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa zamani wa Manchester City, Pep Guardiola, huenda akarejea klabuni hapo hivi karibuni.
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Guardiola raia wa Hispania anatarajiwa kuwa sehemu ya watakaokuwa Etihad kutazama mchezo ujao wa Man City.
Mechi hiyo ni ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG ambayo inatarajiwa kuchezwa Oktoba 14, 2026.
Taarifa zinaeleza kuwa kocha huyo raia wa Hispania ameshawaambia mabosi wa Man City kwamba atakuwepo uwajani siku hiyo.
Guardiola aliondoka Man City mwishoni mwa msimu uliopita baada ya miaka 10 ya kufanya kazi na klabu hiyo. Kwa miaka 10, alitwaa mataji 20.


