MADRID, Hispania
BEKI wa Real Madrid, Marc Cucurella, amesimama na Jose Mourinho akisema bado ni mapema mno kuanza kumkosoa kocha huyo wa kimataifa wa Ureno.
Kwa upande wake, Cucurella amedai kuwa Madrid inapaswa kuzungumziwa baada ya kumalizika kwa msimu huu [2024-25].
Tangu kocha Mourinho aliporejea Santiago Bernabeu, Madrid imefungwa mechi mbili kati ya saba za Ligi Kuu ya Hispania [La Liga] ilizocheza.
Kufungwa na Real Betis na Atletico Madrid kumeifanya Madrid kuzidiwa pointi sita na wapinzani wao wakubwa, Barcelona, ambao wako kileleni mwa msimamo wa La Liga.
“Kwa Madrid, tumeanza na kocha mpya na ni mapema mno kuanza kuzungumzia. Baadhi ya wachezaji walikuwa na wiki moja tu kwenye ‘pre-season’,” amesema Cucurella.


