22.2 C
New York

Uhaba wa maji watesa watu 714,921

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

WATU 714,921 waliotarajiwa kupata maji ya uhakika, hawanufainiki na huduma hiyo, kwa mujibu wa Ripoti ya Taasisi ya Uwajibikaji wa Umma [WAJIBU] ya Mwaka 2024-25.

Katika Ripoti iliyozinduliwa Septemba 25, 2026, WAJIBU imeeleza kuwa kati ya vyanzo 4,007 vilivyopimwa na kuonekana na uhakika wa kutoa huduma ya maji, 516 [13%] havifanyi kazi hiyo, hivyo kuathiri watu 714,921 waliotarajiwa kunufaika.

Pia, Ripoti imeeleza zaidi, kwamba mahitaji ya maji yalikuwa meta za ujazo milioni 85.57 lakini uzalishaji halisi ulikomea mita za ujazito milioni 24.52 pekee, sawa na uhaba wa mita za ujazo milioni 61.04 [71%].

Ripoti inaeleza kuwa kutokana wasichana na wanawake ndiyo waathirika zaidi wa changamoto hiyo kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi na kwenda umbali mrefu kutafuta maji.

Aidha, kwa wanafunziwa kike, hali hiyo imekuwa ikiathiri maendeleo yao kitaaluma kwani hukosa muda wa kwenda shule au kujisomea wawapo nyumbani.

Related articles

Recent articles