16.8 C
New York

Romero aombewa unadhodha Argentina

Published:

LONDON, Uingereza

LEJENDARI Angel Di Maria amemshauri kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Lionel Scaloni, kumkabidhi kitambaa cha unahodha Cristian Romero.

Aidha, kauli hiyo ya Di Maria imekuja baada ya nahodha wa kikosi, Lionel Messi, kustaafu majukumu yake ya kuitumikia timu ya Taifa mwezi uliopita.

Di Maria alikuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2022.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, mkongwe huyo ameeleza kuwa Romero anayekipiga Atletico Madrid ana sifa zote za kuiongoza Argentina.

“Anastahili,” amesema Di Maria na kuongeza: “Nafikiri ni uamuzi mzuri kwa Scaloni na wasaidizi wake wa benchi la ufundi. Anastahili kwa kuwa ni mtu mzuri …” amesema Di Maria.

Related articles

Recent articles