LISBON, Ureno
KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Ureno, Jorge Jesus, ameanika sababu ya kumuweka benchi nahodha wake, Cristiano Ronaldo, katika mchezo dhidi ya Norway.
Timu hizo zilikutana jana Septemba 27, 2026 katika mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya [UEFA Nations League] na Ureno kupata ushindi wa mabao 2-1.
Ronaldo aliishia benchi kwa dakika zote 90 za mechi hiyo, huku nafasi yake kwenye eneo la ushambuliaji ikichukuliwa na Goncalo Ramos aliyefunga bao moja na jingine akipachika Joao Felix.
Akizungumzia sababu ya kumweka benchi ‘CR7’, Jesus amesema aliona staa huyo hawezi kucheza mechi mbili mfululizo baada ya kumpa dakika 70 dhidi ya Wales.
“Tunataka Cristiano Ronaldo awe na sisi katika mechi zote nne, bila kujali anacheza dakika nyingi au chache,” amesema kocha huyo wa zamani wa Al Hilal ya Saudi Arabia.


