13.4 C
New York

Baada ya Kane, Bayern wamgeukia Olise

Published:

MUNICH, Ujerumani

BAADA ya kufanikisha mkataba mpya wa Harry Kane, uongozi wa Bayern Munich umehamishia nguvu kwa mshambuliaji wake mwingine, Michael Olise.

Kane amesaini mkataba utakaombakiza Munich hadi mwaka 2029 baada ya kufunga mabao 73 msimu uliopita na kutwaa tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.

Kama ilivyo kwa Kane, Olise naye ni mchezaji muhimu kwa Bayern tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2024 akitokea England alikokuwa akiitumikia Crystal Palace.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifunga mabao 22 na kutoa asisti 27 msimu uliopita na kwa sasa anawindwa na klabu kadhaa, zikiwamo Arsenal, Real Madrid na Liverpool.

Zipo taarifa zinazodai kuwa mabosi wa klabu ya Madrid wamejipanga na kutenga kitita cha euro milioni 200 kwa ajili ya kumsajili Olise.

Related articles

Recent articles