13.4 C
New York

Liverpool yataka beki wa kushoto Uturuki

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

LIVERPOOL inamtolea macho mlinzi wa kushoto wa Fenerbahce ya Ligi Kuu nchini Uturuki, Archie Brown.

Liverpool wanakumbuka kiwango kizuri alichokionesha Brown wakati timu yao ilipotandikwa mabao 24 na Fenerbahce katika mechi iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Istanbul, Uturuki, nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga bao moja na kutoa ‘asisti’.

Hata hivyo, mabosi wa Liverpool wanafahamu kuwa hawako peke yao kwani tayari Chelsea, Newcastle United, Everton, Brighton na AC Milan nazo zimeonesha kumtaka nyota huyo.

Lakini, kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uturuki, mchezaji huyo anavutiwa zaidi kwenda England, licha ya kwamba bado anatamani kubaki Uturuki.

Related articles

Recent articles