17.5 C
New York

Messi ashika nafasi ya pili ‘mipira iliyokufa’

Published:

LONDON, Uingereza

LIONEL Messi anashika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa mabao ya mipira ya kutenga katika historia ya soka.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Argentina amefikisha mabao 75, wakati Ronaldo anashika nafasi ya tisa akiwa na mabao 63.

Kwa mwaka 2026 pekee, Messi anayeitumikia Inter Miami ya Ligi Kuu ya Marekani [MLS] ameshafunga mara sita kwa mipira ya kutenga.

Akiwa na mabao yake 75, Messi amewapiku wakongwe Juninho Pernambucano (72), Roberto Dinamite (73) na Jair (74).

Hata hivyo, kwa sasa mchezaji anayeongoza kwa mabao mengi ya mipira ya kutenga ni kiungo raia wa Brazil, Marcelinho Carioca, ambaye alistaafu akiwa na 78.

Related articles

Recent articles