22.1 C
New York

Straika aondoka United, atua Uholanzi

Published:

MANCHESTER, Uingereza

STRAIKA Chido Obi ameondoka rasmi katika klabu ya Manchester United na kujiunga na Willem II ya Uholanzi kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja.

Chido Obi alikuwa sehemu ya kikosi cha Man United katika maandalizi ya msimu (pre-season) lakini zilikuwepo taarifa kuwa angeondoka.

Hata hivyo, bado Man United imeonesha kuwa na imani na kiwango chake, hivyo huenda akarejea msimu ujao (2027-28).

Katika mkataba wake wa mkopo, Man United hawajaweka kipengele kinachoiruhusu Willem II kumsajili moja kwa moja hapo baadaye.

Related articles

Recent articles