22.5 C
New York

Iran, Marekani zashambuliana tena

Published:

TEHRAN, Iran

KWA mara ya kwanza baada ya wiki mbili, Iran na Marekani zimeshambuliana katika Mlango-Bahari wa Hormuz.

Kwa mujibu wa taarifa, vikosi vya kijeshi vya Marekani ndivyo vilivyofanya mashambulizi kwa meli za Iran.

Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la Iran (IRGC), shambulizi hilo limeua watu wawili na kujeruhi wengine wawili.

Marekani, kwa upande wao, wamedai kuwa walifanya shambulizi hilo baada ya kubaini kuwa Iran ilishajipanga kushambulia.

Katika hatua nyingine, Iran imedai kuwa imelipiza kisasi kwa kushambulia kambi za Marekani zilizoko nchini Jordan.

Related articles

Recent articles