WASHINGTON DC, Marekani
DENI la Taifa la Marekani limefikia Dola trilioni 40, kiasi kikubwa zaidi cha fedha katika historia ya nchi hiyo, huku lawama zikielezwa katika matumizi makubwa ya jeshi.
Aidha, deni hilo limeongeza kutoka Dola trilioni 39 zilizoripotiwa Machi, 2026, na Dola milioni 38 miezi mitano kabla, kwa maana ya Oktoba, 2025.
Kuhusu matumizi makubwa ya kijeshi, utawala wa Rais Donald Trump unatupiwa lawama kwa vita vyake na Iran vilidumu kwa takribani miezi sita.
Hata hicho, Msemaji wa Serikali, Kush Desai, amesema utawala wa Rais Trump inajikita katika kuondosha matumizi yasiyo ya lazima na vitendo vya rushwa ili kupunguza Deni la Taifa.
Kwa upande wao, wataalamu wa uchumi wamedai kuwa kinachotokea kwa Rais Trump na hata marais wengine wa Marekani kwa miaka ya hivi karibuni ni matumizi makubwa kuliko kiasi cha kodi kinachokusanywa.
Wakati huo huo, wachambuzi wamedai kuwa kupanda kwa Deni la Taifa kumeanza kuathiri moja kwa moja maisha ya wananchi wa Marekani.


