27.1 C
New York

Lebanon yamkabidhi mshirika wa Al-Assad

Published:

BEIRUT, Lebanon

MAMLAKA za Lebanon zimemkamata na kumkabidhi nchini Syria aliyekuwa jenerali wa jeshi wakati wa utawala wa Rais Bashar al-Assad.

Meja Jenerali huyo, Adel Issa, anashitakiwa nchini Syria kwa makosa ya uhalifu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2024.

Kama itakumbukwa, Adel Issa (67), pamoja na Rais Assad walikimbia nchini humo baada ya utawala wao kuangushwa.

Adel Issa alikamatwa Agosti 8, 2026 alipotembelea ofisi za ubalozi wa Syria mjini Beirut, Lebanon. Amerejeshwa jana Agosti 19, 2026.

Hatua ya Lebanon kumkabidhi imetokana na presha kubwa iliyopewa na mamlaka za Syria, ikiitaka kumkabidhi ili akajibu mashitaka.

Kwa upande wake, mamlaka za Syria zimedai kuwa Adel Issa aliongoza operesheni za kijeshi katika Jimbo la Mashariki la Deir Ezzor hadi mwaka 2016.

Mashitaka yanayomkabili ni pamoja na kuteka, kutesa na kuua waasi waliokuwa wakipinga Serikali ya Rais Assad.

Related articles

Recent articles