LONDON, Uingereza
ZIPO taarifa zinazodai kuwa Victor Osimhen wa Galatasaray ni miongoni mwa mastraika walio kwenye orodha ya kocha wa Arsenal, Mikel Arteta.
Gazeti la UK Telegraph limeripoti kuwa Arsenal kwa sasa wanamtazama zaidi Osimhen kuliko mshambuliaji wa kati wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Washika Bunduki wameona imekuwa ngumu kwa Atletico Madrid kumwachia Alvarez, achilia mbali thamani yake ya Pauni milioni 100.
Arsenal wanaamini huenda Alvarez akavutiwa zaidi na Barcelona, ambayo pia inamtaka akazibe pengo la Robert Lewandowski aliyekimbilia Ligi Kuu ya Marekani (MLS).
Osimhen (27), ni moja ya washambuliaji wa kati tishio kwa sasa barani Ulaya, alithibitisha hilo akiwa na Napoli, kabla ya kuhamia Galatasaray ya Uturuki.


