28.1 C
New York

Nigeria yakosa tiketi Kombe la Dunia 2027

Published:

RABAT, Morocco

TIMU ya soka ya Taifa ya Nigeria ya Wanawake ‘Super Falcons’ haitoshiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2027.

Super Falcons wamepoteza nafasi hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Afrika Kusini ‘Banyana Banyana’.

Hilo ni pigo jingine kwao kwa hivi karibuni baada ya safari yao kuishia hatua ya robo fainali katika michuano ya WAFCON (fainali za AFCON za Wanawake).

Ni michuano ambayo Super Falcons imekuwa na utawala mkubwa, ikiongozwa kwa kutwaa ubingwa wake mara 10.

Dhidi ya Afrika Kusini, Super Falcons waliweza kukomaa kwa suluhu hadi mapumziko, kabla ya kuruhusu mabao mawili ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Thembi Kgatlana na Refiloe Jane.

Related articles

Recent articles