MADRID, Hispania
VIGOGO wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Real Madrid, wako mbioni kuwapiga bei mastaa wao wawili, Ferland Mendy na Raul Asencio.
Madrid wamepoteza imani na Mendy kutokana na majeraha yake ya mara kwa mara, wakati Asencio ameshindwa kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza.
Licha ya mpango wake huo, Madrid haijapokea ofa yoyote kwa wachezaji hao, ingawa zipo tetesi zinazowahusisha na klabu mbalimbali za ndani na nje ya Hispania.
Mendy amekuwa akihusishwa zaidi na Aston Villa ya Ligi Kuu ya England (EPL), wakati Asencio anatajwa kuwa kwenye rada za Atletico Madrid.
Kwa mujibu wa ripoti, kuondoka kwao Santiago Bernabeu ni sehemu ya mipango ya kocha Jose Mourinho kuimarisha kikosi kwa ajili ya msimu ujao (2026-27).


