30 C
New York

Zidane amvuta Barthez, apewa ajira Ufaransa

Published:

PARIS, Ufaransa

MLINDA mlango wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Fabien Barthez, ameajiriwa kuwa sehemu ya wasaidizi wa kocha mkuu wa kikosi hicho, Zinedine Zidane.

Kwa mujibu wa taarifa, Barthez anakwenda kwenye benchi kumsaidia ‘Zizou’ katika majukumu ya kuwanoa makipa wa timu hiyo.

Zidane aliajiriwa wiki chache zilizopita na kusaini mkataba wa miaka minne kuinoa Les Bleus akichukua nafasi ya Didier Deschamps aliyejizulu baada ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026).

Barthez, Zidane na Deschamps walikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichocheza na kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 na fainali za EURO mwaka 2000.

Kwa upande wake, Barthez alicheza mechi 87 akiwa na Ufaransa, ya mwisho ikiwa ni ile ya fainali ya Kombe la Dunia za mwaka 2006.

Katika mchezo huo dhidi ya Italia, Zidane alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa beki Marco Materazzi.

Katika ngazi ya klabu, Barthez mwenye umri wa miaka 55 aliwahi kuzitumikia Toulouse, Marseille, Manchester United na Monaco.

Related articles

Recent articles