27.5 C
New York

Motsepe aibuka kumkingia kifua Infantino

Published:

CAIRO, Misri

RAIS wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amesema hakuna namna ya kumng’oa Gianni Infantino ndani ya FIFA zaidi ya kusubiri Uchaguzi.

Motsepe amekuja na kauli hiyo wakati huu Rais huyo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) akikabiliwa na shinikizo la kujiuzulu baada ya jaribio lake la kuuza hisa za Kombe la Dunia.

Infantino haungwi mkono na mashirikisho ya soka ya Ulaya (UEFA), Asia (AFC) na Amerika (CONCACAF), ambayo yanamtaja kama ‘kiongozi aliyefeli’.

Kwa pamoja, viongozi wa mashirikisho hayo wamemjia juu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 wakimtaka kujiuzulu na kuachana na mpango wa kugombea urais katika Uchaguzi ujao wa Machi, 2027.

Hata hivyo, Motsepe ambaye ni Makamu wa Rais wa FIFA, amesema bosi wake hawezi kuondoshwa kwenye nafasi hiyo bila kufuata mchakato, ambao ni kura za wanachama kupitia Uchaguzi.

“Kama unataka aondoke, nenda kwenye Uchaguzi; acha wajumbe 211 waamue,” amesema Motsepe, ambaye nje ya soka, ni mfanyabiashara tajiri nchini Afrika Kusini.

Related articles

Recent articles