30.4 C
New York

Kenya yataka uenyeji mashindano ya Riadha ya Dunia

Published:

NAIROBI, Kenya

KENYA imetupa karata yake katika mbio za kuwania tiketi ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Riadha ya Dunia yatakayofanyika mwaka 2029.

Endapo Kenya itafanikiwa katika mpango wake huo, basi itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuandaa michuano hiyo.

Hata hivyo, Kenya inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Uingereza, Italia na Ujerumani, huku mshindi akitarajiwa kutangazwa Septemba, 2026.

Taarifa zinaeleza kuwa Kenya inauangalia Uwanja wake wa Kasarani ulioko Mji Mkuu wa Nairobi kuwa ndiyo utakaotumika kwa mashindano hayo.

Related articles

Recent articles