LOS ANGELES, Marekani
MAGARI zaidi ya 650,000 yaliibiwa nchini Marekani mwaka 2025, licha ya kwamba idadi ya matukio hayo imepungua katika miaka ya hivi karibuni.
Wakati huo huo, inaeleza kuwa magari aina ya Hyundai Elantra ndiyo yanayoongoza kwa kuibiwa (21,732 kwa mwaka 2025), yakifuatiwa na Honda Accord (17,797).
Kwa mujibu wa Shirika la Uhalifu wa Bima la Marekani (NICB), Jimbo la California ndilo linaloongoza kwa matukio ya wizi wa magari nchini humo.
Kwa California, wastani wa matukio ya wizi wa magari ni 348 katika kila wakazi 100,000, kwa mujibu wa ripoti ya NICB kwa takwimu za mwaka 2025.
Aidha, Nevada inashika nafasi ya pili ikiwa na wastani wa wizi wa magari 318 katika kila watu 100,000, kama ilivyo kwa Jimbo jingine la Marekani, New Mexico.
Jimbo la Missouri linafuata likiwa na wizi wa magari 280 katika kila watu 100,000, kama ilivyo pia kwa Colorado, ikifuatiwa na Maryland (273), Texas (240), na Alaska (232).
Majimbo mengine na wastani wake wa matukio ya wizi wa magari ni kama ifuatavyo: Washington (228), Illinois (223), Oregon (208), Kansas (201), Tennessee na Louisiana (188), North Carolina (185), South Carolina (184), na Ohio (174).
Hata hivyo, New Hampshire ndilo Jimbo lenye kiwango kidogo cha matukio ya wizi wa magari, ambapo ni wastani wa 40 katika kila wakazi 100,000.


