WASHINGTON DC, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema wanatarajia kukaa mezani na viongozi wa Iran kujadili mustakabali wa vita vyao vilivyoanza Febrauri 28, 2026.
Kwa mujibu wa Rais Trump, mazungumzo ya pande mbili hizo yanatarajiwa kufanyika leo Agosti 3, 2026, akidai kuwa ndiyo sababu ya Marekani kusitisha shambulizi kubwa ililotarajia kufanya nchini Iran.
“(Iran) wanajua ukubwa na madhara ya shambulizi hilo kwa sababu waliona maandalizi yake. Tunazungumza nao kuona tunavyoweza kufikia makubaliano. Yataanza kesho mchana (leo),” amesema.
Kabla ya kuja na kauli hiyo, Rais Trump alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Truth Social kusema washirika wao wa Mashariki ya Kati wamewaomba wasifanye shambulizi na badala yake wakae mezani na Iran.
Kwa upande wake, Iran haijazungumzia chochote juu ya Rais Trump kudai kuwa kutakuwa na mazungumzo, licha ya kiongozi huyo kusisitiza kuwa vita viko ukingoni kumalizika.


