28 C
New York

Argentina, Uingereza zinagombea Visiwa hivi

Published:

LONDON, Uingereza

‘MALVINA ni Argentina’ ni ujumbe uliosomeka katika bango walilobeba wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina baada ya kuifunga England katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu (2026).

Malvina kwa lugha ya Kiargentina, ikimaanisha Visiwa vya Falkland vilivyoko Kusini mwa Bahari ya Atlantic. Argentina na Uingereza zimekuwa zikigombea udhibiti wa Kisiwa hicho na ziliwahi kuingia kwenye vita ya siku 10 mwaka 1982.

Tangu wachezaji wa Argentina walipoonesha bango lao, ujumbe huo wa ‘Malvina ni Argentina’ umejizolea umaarufu mkubwa nchini humo, ikiwamo kuchapishwa katika T-shirt, viatu, mabegi, na hata jezi za soka.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba hakuna mchezaji wa sasa wa timu ya Taifa ya Argentina aliyekuwa amezaliwa wakati Serikali ya kidikteta ilipoivamia Kisiwa cha Falkland mwaka 1982.

Argentina iliviteka Visiwa hivyo kwa siku 73, kabla ya wanajeshi wa Uingereza kuvamia na kuzuka kwa vita vya siku 10 vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 900. Uingereza ilishinda vita hivyo.

Tangu hapo, kumekuwapo na uadui wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo na imetokea mara kadhaa kwa Argentina kuvitaja Visiwa hivyo katika mechi zake dhidi ya Uingereza.

Katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1986, Diego Maradona alisema mabao mawili aliyoifunga Uingereza kwenye mchezo wa robo fainali ni kisasi kwa kile wapiganaji wao waliopoteza maisha katika vita vya mwaka 1982.

Visiwa vya Falkland vina wakazi wapatao 3,600, huku ufugaji wa kondoo ukiwa wa kiwango kikubwa. Tangu wachezaji wa Argentina walipoonesha bango, ufuatiliaji wa Visiwa hivyo kupitia Google umeongezeka kwa asilimia 2,400.

Wakati huo huo, Chama cha Soka cha Argentina kimeingia matatizoni baada ya kufunguliwa mashitaka juu ya timu yake kujihusisha na siasa kinyume cha sheria za FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).

Related articles

Recent articles