28.4 C
New York

Rais Ukraine awasili Uingereza

Published:

LONDON, Uingereza

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amewasili nchini Uingereza, ambako atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu mpya, Andy Burnham.

Zelensky atakuwa mgeni wa kwanza wa nje kufika Uingereza tangu Burnham alipoingia madarakani siku chache zilizopita.

Burnham ameahidi kuwa Uingereza itaendelea kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi vilivyoanza Februari, 2022.

Kabla ya kuwasili Uingereza, Zelensky alishaweka wazi kuwa Uingereza na Taifa lake wana uhusiano mkubwa na wa kihistoria.

Kwa upande wake, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imekuwa sehemu ya washauri muhimu wa Ukraine, hasa katika kuikabili Urusi ambayo imetengwa na mataifa mengi ya Ulaya.

Related articles

Recent articles