19.7 C
New York

Simba yaipiga bao Yanga, yamtambulisha Keletso

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

BAO la kisigino! Ndivyo unavyoweza kuita baada ya Simba kumtanbulisha winga wa kimataifa wa Afrika Kusini, Keletso Makgalwa.

Nyota huyo aliyecheza Sekhukhune United msimu uliopita, alikuwa kwenye rada za mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga, kabla ya Simba kukatiza mbele na kupita naye.

Keletso mwenye umri wa miaka 29, ni moja ya wachezaji wenye majina makubwa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, akiwahi pia kuitumikia Mamelodi Sundowns.

Wakala wake, Ntobatsi Masegela, amefichua kuwa Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kufika mezani, hivyo walivutiwa na jitihada zao.

“Pia, Simba walikuja na mkataba wenye mipango ya muda mrefu. Ni wazi siwezi kusema unahusu nini lakini hicho pia kilichangia uhamisho wake,” amesema Ntobatsi.

Mbali na Yanga, Kaizer Chiefs ni klabu nyingine kubwa barani Afrika iliyokuwa kwenye mbio za kuiwania saini ya mchezaji huyo.

Related articles

Recent articles