17.4 C
New York

Newcastle hesabu zote kwa kipa Man City

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Newcastle United iko mstari wa mbele katika mbio za kumsajili mlinda mlango wa Manchester City raia wa England, James Trafford.

Newcastle imemuongeza kipa chipukizi kutoka Reims, Ewen Jaouen, lakini bado inataka mwingine wa kumpa changamoto Nick Pope.

Itakumbukwa, Newcastle walijaribu kumsajili Trafford mwaka jana lakini aliamua kujiunga na Manchester City akitokea Burnley.

Hata hivyo, mambo yamekuwa magumu kwa staa huyo mwenye umri wa miaka 23, ambapo amemaliza msimu wa 2025-26 akiwa amecheza mechi 17 pekee.

Ugumu wa Trafford kupata namba pale Etihad umetokana na uwepo wa kipa wa daraja la juu raia wa Italia, Gianluigi Donnarumma.

Related articles

Recent articles