18.4 C
New York

Arsenal wanamtaka huyu kutoka La Liga

Published:

LONDON, Uingereza

MABINGWA wa Ligi Kuu ya England (EPL), Arsenal, wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Real Sociedad ya La Liga, Ander Barrenetxea.

Ripoti zinaeleza kuwa tayari Mkurugenzi wa Michezo wa Washika Bunduki hao, Andrea Berta, ameshaingia mzigoni kuhakikisha nyota huyo atapatikana kwa ajili ya msimu ujao.

Barrenetxea aliumaliza msimu wa 2025-26 wa La Liga akiwa ameingia kambani mara nne na kutoa asisti tano katika mechi 30.

Pia, nyota huyo aliyetokea katika ‘academy’ ya Sociedad ndiye aliyefunga bao la kwanza wakati timu hiyo ilipoifunga Atletico Madrid na kutwaa ubingwa wa Copa del Rey mwaka huu (2026).

Majeraha ya mwishoni mwa msimu huo yalimfanya akose kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania kilichokwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea huko Marekani, Mexico na Canada.

Sociedad, kwa upande wao, wanataka kumbakiza mchezaji huyo kikosini kwa ajili ya msimu ujao lakini wanaweza kumwachia endapo tu watawekewa mezani kitita cha Pauni milioni 65.

Related articles

Recent articles