30 C
New York

Rais mstaafu Colombia amjia juu Trump

Published:

BOGOTA, Colombia

RAIS aliyemaliza muda wake nchini Colombia, Gustavo Petro, amemnyooshea kidole Donald Trump wa Marekani kwa hatua yake ya kumuunga mkono mgombea wa urais Abelardo de la Espriella.

De la Espriella (47), amemzidi kura Seneta Ivan Cepeda katika kinyang’anyiro cha urais baada ya Uchaguzi Mkuu wa Jumapili ya wiki iliyopita, lakini warudiana Juni 21, 2026.

Kwa upande wake, Petro anamtaja De la Espriella kuwa ni mfanyabishara wa dawa za kulevya asiyepaswa kupewa nafasi ya kwenda Ikulu.

Wakati huo huo, amelaani kitendo cha Marekani kuingilia chaguzi la Latini ya Amerika, hasa kampeni za uchaguzi za Colombia.

Hata hivyo, mtazamo wake ni tofauti na alionao Trump, ambaye anamtaja De la Espriella kuwa ni mtu sahihi wa kuingia madarakani. Go

Related articles

Recent articles