25.3 C
New York

Mbu watajwa kuongoza vifo vya binadamu duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

HIYO ni kwa mujibu wa takwimu za tovuti ya Our World in Data, kwamba mbu ndiyo wadudu/wanyama wanaosababisha vifo vingi vya binadamu. Vifo 760,000 kwa mwaka.

Kwa mujibu Our World in Data, mbu hueneza magonjwa ya malaria, dengue na homa ya manjano, ambayo kwa pamoja husababisha idadi hiyo ya vifo.

Itakumbukwa kuwa Ripoti ya mwaka 2022 ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) ilionesha kuwa Malaria peke yake ilisababisha vifo 600,000.

Katika Ripoti hiyo, WHO ilieleza kuwa mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara yako hatarini zaidi katika vita dhidi ya ugonjwa huo.

Ukiweka mbali mbu, wadudu wengine waliotajwa kushika nafasi ya pili ni nyoka, ikielezwa kuwa sumu yake ni chanzo cha vifo 100,000 kila mwaka.

Wanyama aina ya mbwa, licha ya kupewa jukumu la ulinzi katika jamii nyingi, nao wametajwa kuchangia vifo vya watu 40,000 ndani ya kipindi hicho cha mwaka mmoja.

Aidha, vijidudu vinavyosabaisha uchafuzi wa maji safi, wakiwamo konokono, vimeelezwa pia kuchangia vifo 14,000 (kila mwaka) vitokanavyo na ugonjwa wa kichocho.

Related articles

Recent articles