LONDON, Uingereza
KATIKA dakika ya 89 ya mchezo wa Championship dhidi ya Millwall, kiungo wa West Ham United, Mohamadou Kante, alifanya aliwakosha mashabiki na wachezaji wenzake baada ya kucheza rafu iliyomsababishia kadi nyekundu.
Ikiwa ni ‘derby ya London’, Kante hakuwa na namna zaidi ya kumwangusha kwenye boksi Kyrell Lisbie aliyekuwa anaelekea kufunga bao.
Kante, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20, alifanya hivyo wakati timu hizo zikiwa sare ya mabao 2-2, hivyo kama angemwacha Lisbie afunge, basi wangepoteza mchezo huo.
Baada ya kadi nyekundu hiyo, nyota huyo alipongezwa na wachezaji wenzake, pia mashabiki wa West Ham waliokuwa jukwaani walionesha kukoshwa na alichokifanya.
Mchezo huo uliiishuhudia Millwall ikitangulia kwa mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Caleb Taylor na Camiel Neghli, kabla ya West Ham kusawazisha yote kipindi cha pili.


