18.6 C
New York

Liverpool, City zamtolea macho Aramburu

Published:

LONDON, Uingereza

BEKI wa Real Sociedad ya La Liga, Jon Aramburu, ameingia kwenye rada za klabu kubwa mbili za Ligi Kuu ya England [EPL], Liverpool na Manchester City.

Aramburu, raia wa Venezuela mwenye umri wa miaka 24, ni kiraka wa eneo la ulinzi kwani licha ya kucheza beki wa kulia, pia amekuwa akitumika kushoto.

Man Ciy ilihitaji beki wa aina hiyo wakati wa usajili wa kiangazi, mwaka huu, ambapo ilihusishwa zaidi na Malo Gusto [Chelsea] na Timo Livramento [Tottenham].

Kwa upande mwingine, klabu za Tottenham, Newcastle United, Everton na Fulham nazo zimeripotiwa kuitaka saini ya nyota huyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Aramburu ana thamani ya Pauni milioni 50 katika mkataba wake na Real Sociedad utakaofikia ukomo mwaka 2030.

Related articles

Recent articles