18.6 C
New York

Wirtz kulamba mkataba mpya Anfield

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

KLABU ya Liverpool iko mbioni kumpa mkataba mpya kiungo wake raia wa Ujerumani, Florian Wirtz, licha ya kusuasua kwa kiwango chake.

Nyota huyo hajafunga bao katika mechi 12 alizocheza hivi karibuni akiwa na Liverpool na timu yake ya Taifa ya Ujerumani.

Hata hivyo, licha ya kuwindwa na klabu kadhaa, ripoti zinaeleza kuwa Liverpool haina mpango wa kuachana na nyota huyo.

Kocha wa Liverpool, Andoni Iraola, anamuona nyota huyo aliyesajiliwa kwa Pauni milioni 116 kama mchezaji muhimu kwenye mipango yake.

Ikumbukwe, saini yake ilihusishwa na klabu kadhaa, zikiwamo PSG na Atletico Madrid, wakati wa usajili wa dirisha kubwa lililofungwa wiki chache zilizopita.

Related articles

Recent articles