16.4 C
New York

Vita ya Iran: Wakurdi walimsaliti Trump?

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS Donald Trump ameendelea kuwashutumu wapiganaji wa jamii ya Wakurdi akidai kuwa walificha silaha walizopewa na Marekani wakati wa maandamano makubwa ya raia nchini Iran.

Kwa madai yake, Marekani iliwapa Wakurdi silaha za kuwapatia waandamaanaji waliokuwa mitaani kupinga utawala wa Serikali ya Iran iliyoko madarakani.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Rais Trump, msaada huo wa Marekani ulilenga kuwasaidia raia kukabiliana na vyombo vya dola vilivyokuwa vikitumia risasi za moto kudhibiti maandamano.

Rais Trump amesema licha ya Wakurdi kupokea bunduki na mabomu kutoka Marekani, hawakuzifikisha silaha hizo kwa raia, hivyo Serikali ya Iran kufanikiwa kuzima maandamano na kuendelea kutawala.

“Tulituma silaha kwa waandamaanaji, silaha nyingi tu. Nafikiri Wakurdi walichukua silaha na kukaa nazo. Inasikitisha, zilipaswa kuwafikia raia,” amesema.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa za Mashariki ya Kati wanasema madai hayo yanaonesha namna Rais Trump alivyo na uelewa mdogo juu ya jamii ya Wakurdi.

Kwa wachambuzi wa siasa za Mashariki ya Kati, Rais Trump anawataja Wakurdi kama kundi moja, wakati ni jamii iliyoenea katika nchi za Uturuki, Syria, Iraq na Iran.

Wachambuzi wanasema Rais Trump anatupa lawama kwa Wakurdi lakini ameshindwa kueleza ni jamii ipi kati ya hizo alizoipa silaha anazodai kutolewa na Marekani.

Dkt. Kamran Matin ni muhadhiri wa taaluma yaMahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Sussex, anasema: “Trump ana uelewa mdogo juu ya jamii ya Wakurdi na siasa zao.”

Kwa upande wa Wakurdi wa Iran, kikiwamo Chama cha siasa cha Free Life Party of Kurdistan (PJAK), wamekanusha madai hayo ya kupokea silaha za Marekani.

Ni kama ambavyo Chama jingine cha Wakurdi nchini Iran, Komala, kimesema kauli za Rais Trump zinathibitisha alivyochanganyikiwa na vita dhidi ya Iran.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Fariba Mohammadi, amesema hakuna kundi la Wakurdi, kwa maana ya vyama vya siasa au wapiganaji, kilichotokea silaha kutoka kwa Marekani.

Juu ya madai ya Rais Trump, Kamal Chomani, ambaye ni Mhariri Mkuu wa Gazeti la Amargi linaloripoti masuala ya Mashariki ya Kati, anasema Rais Trump anatafuta visingizio baada ya kukwama katika mpango wake wa kuuondosha utawala wa Iran.

Chomani amesema Rais Trump alishawishiwa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwamba lingekuwa ni suala la muda mfupi tu kuangusha utawala wa Iran.

“Mpango huo ulipofeli, Trump ameanza kutafuta visingizio. Kuficha udhaifu wake, anaitumia jamii ya Wakurdi kama kisingizio. Hakuna silaha zilizotumwa kwa Wakurdi ili kusambazwa kwa wananchi ndani ya Iran.

“Tunaona kabisa kwamba hata usambazaji wa setilaiti za intaneti (baada ya Iran kuzima) ulikumbana na changamoto, achilia mbali hilo la kupitisha silaha,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img