WASHINGTON DC, Marekani
MJADALA wa nani atakuwa Rais ajaye wa Marekani umepamba moto si tu nje, bali hata ndani ya korido za Ikuku ya Marekani. Ni Katibu Mkuu wa Ikulu, Marco Rubio, au Makamu wa Rais, JD Vance?
Kwa pamoja, wawili hao wamekuwa na ushawishi mkubwa ndani na hata nje ya Chama chao cha Republican, hivyo kuongeza joto la mjadala wa nani atakayepitishwa kukalia kiti cha Rais Trump.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa Mei 15-18, 2026, asilimia 34 ya wananchi wa Marekani waliohojiwa walimtaja JD Vance kuwa ndiye mtu sahihi zaidi wa kuiongoza nchi hiyo baada ya Rais Trump.
Rubio alipata asilimia 33. Kabla ya matokeo hayo, ulikuwepo utafiti mwingine wa Januari, 2025, ambapo JD Vance pia aliongoza kwa asilimia 42.
Hivi karibuni, Rais Trump aliongeza upana wa mjadala wa nani atakuwa mrithi wake mwaka 2028. Akihutubia, aliuliza wananchi juu ya nani wanayemtaka kati ya JD Vance na Rubio.
Rubio, ambaye akiingia Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2010, alikuwa mashindani wa Rais Trump katika Uchaguzi wa ndani wa Chama cha Republican mwaka 2016 lakini alishindwa.

Akawa mgombea mwenza wa Rais Trump na tangu hapo amekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya Chama kwa namna anavyosimamia na kutekeleza sera za Serikali iliyoko madarakani.
Kwa upande wake, Rubio naye amekuwa sehemu muhimu ya utawala wa Trump na hivi karibuni alifunga safari hadi Vatican na kukutana na Papa Leo, ambaye amekuwa na uhusiano usio na afya na Rais huyo.
Katika ziara hiyo, Rubio alikutana pia na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, ambaye inafahamika kuwa ni mmoja ya washirika wakubwa wa Rais Trump.
Licha ya ushawishi wao huo, wote na kwa nyakati tofauti, wamekuwa wakijiweka mbali na taarifa za kuhusishwa na nafasi hiyo ya urais.
“Mimi siyo mgombea wa urais. Mimi ni Makamu wa Rais na naipenda kazi yangu. Najaribu kufanya kila kilicho kizuri kwa ajili ya kazi yangu,” alisema JD Vance katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari.
Pia, licha ya mjadala wa nani atakuwa Rais, Vance na Rubio wamekuwa wakisisitiza kuwa wao siyo maadui. Rubio amesema atamuunga mkono JD Vance endapo itatokea akachaguliwa kuwa mgombea wa urais katika Uchaguzi ujao wa mwaka 2028.
Kwa upande wake, Rais Trump hajaonesha upande wa nani anamuunga mkono, na badala yake amesema yeyote kati yao ni ‘karata dume’ kwa Chama chake cha Republican.
Hata hivyo, wadadisi wa mambo wanamuona Rais Trump akivutiwa zaidi na Makamu wake, JD Vance, aliamini ndiye mtu sahihi wa kuvaa viatu vyake.


