25.4 C
New York

Cuba yanunua ‘drones’ 300 kuitisha Marekani

Published:

HAVANA, Cuba

SERIKALI ya Cuba imeagiza ndege zisizo na rubani (drones) zaidi ya 300 wakati huu uhusiano wake na Marekani ukiwa kwenye hali mbaya.

Mataifa hayo hayana maelewano mazuri na Rais wa Marekani, Donald Trump, ametishia mara kadhaa kukivamia Kisiwa hicho.

Hatua ya Cuba kununua ndege hizo imetafsiriwa kuwa ni kujiandaa na lolote linaloweza kutokea, hasa endapo Rais Trump atajaribu kutimiza mpango wake huo.

Katika hatua nyingine, Gazeti la Axios la Cuba limeripoti kuwa ununuzi wa ndege hizo ni maandalizi ya kushambulia kambi ya kijeshi ya Marekani iliyoko Guantanamo Bay.

Kwa upande mwingine, Serikali ya Marekani imetajwa kuingiwa na wasiwasi baada ya kuona viongozi wa Iran wakiitembelea Cuba katika siku za hivi karibuni.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img