10.5 C
New York

Upinzani kumng’oa madarakani Benjamin Netanyahu?

Published:

JERUSALEM, Israel

WAZIRI Mkuu wa Israel, Banjamin Netanyahu, anakabiliwa na upinzani mkali katika Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika mwishoni mwa Oktoba, 2026.

Ni baada ya vyama vikubwa viwili vya upinzani nchini humo kuungana, lengo likiwa ni kumng’oa madarakani.

Vyama vilivyounganisha nguvu ni Bennett 2026 cha Naftali Bennett na There is a Future cha Yair Lapid, wote wakiwahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu kwa nyakati tofauti.

Lapid amezungumzia muungano huo akisema umelenga kuiondosha madarakani Serikali ya Netanyahu.

“Hatua hii imelenga kuunganisha nguvu, kuondosha mgawanyiko, na kuelekea nguvu katika kutafuta ushindi katika Uchaguzi muhimu ujao, ili kuipa maendeleo Israel,” amesema.

Taarifa rasmi zilizothibitishwa na Ofisi ya Chama cha Bennett 2026 imeeleza kuwa Muungano wao utafahamika kwa jina la ‘Together’ (Pamoja).

Muungano huo unajaribu kumng’oa madarakani Waziri Netanyahu, ambaye anaiongoza Israel baada ya ushindi wake wa mwaka Novemba, 2022.

Kwa sasa, Waziri huyo anapitia ukosolewaji wa kiwango kikubwa kutokana na ushiriki wa Israel katika migogoro ya Mashariki ya Kati.

Mbali ya mgogoro wake na Iran, Isarel ina uhusiano mbaya, ikiwamo kushambuliana, na vikundi viwili vinavyoihusishwa na ugaidi, Hamas na Hezbollah.

Hamas ni wapiganaji wanaojinasibu kulinda masilahi ya Palestina, wakati Hezbollah ni kikundi cha Lebanon.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Netanyahu ameanza kupoteza ushawishi wake mbele ya makundi mbalimbali, hasa wafanyabiashara wakubwa nchini humo.

Wafanyabiashara, ambao sasa wanatajwa kuunga mkono upinzani, wamekuwa wakilalamikia ongezeko la kodi, wakiamini Serikali inaelekeza fedha nyingi katika vita.

Ni kutokana na mazingira hao, tafiti mbalimbali zinautabiria anguko uongozi wa Waziri Netanyahu katika Uchaguzi Mkuu huo uliobakiza miezi takribani sita kufanyika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img