9.5 C
New York

Trump aitishia kuiangamiza Iran ikiwa Hormuz haitafunguliwa

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameionya Iran kuwa inaweza “kuangamizwa ndani ya usiku mmoja” endapo haitafikia makubaliano kabla ya muda wa mwisho alioweka wa kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani.

Muda huo wa mwisho umewekwa saa 20:00 kwa saa za Washington DC siku ya Jumanne (00:00 GMT Jumatano), ambapo Trump anasisitiza kuwa makubaliano yanapaswa kuruhusu usafirishaji huru wa mafuta kupitia Ghuba.

Akizungumza Ikulu ya White House akiwa na viongozi wa kijeshi, Trump amesema anaamini baadhi ya viongozi wa Iran wanaonyesha nia njema katika mazungumzo, lakini hatma yake bado haijulikani.

“Nchi nzima inaweza kuangamizwa kwa usiku mmoja,” alionya Trump, akiongeza kuwa Iran inaweza kurudishwa katika hali ya “Enzi ya Mawe” iwapo haitatii.

Hata hivyo, Iran imekataa pendekezo la kusitisha mapigano kwa muda, ikitaka kumalizika kabisa kwa vita pamoja na kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi.

Wakati huo huo, juhudi za upatanishi zinaendelea zikihusisha mataifa ya Pakistan, Uturuki na Misri, huku changamoto ya mawasiliano ikitajwa kuwa kikwazo kikubwa katika mazungumzo hayo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img