22 C
New York

Uingereza: “Hii sio vita yetu, hatutajiingiza”

Published:

LONDON, Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, amesema wazi kuwa nchi yake haitapeleka wanajeshi nchini Iran, akisisitiza kuwa Uingereza haitajiingiza moja kwa moja katika vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati.

Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii, Starmer alikanusha uwezekano wa kushiriki kijeshi katika mzozo huo, akisisitiza kuwa msimamo wa serikali yake unabaki kuwa wa kujilinda na kulinda maslahi ya taifa.

“Hii si vita yetu na hatutajiingiza,” amesema Starmer.

Hata hivyo, alibainisha kuwa Uingereza itaendelea kuchukua hatua za tahadhari kulinda usalama wa raia wake na kulinda maslahi ya nchi pamoja na washirika wake katika eneo hilo.

“Tunachukua hatua za kujilinda ili kulinda maisha ya Waingereza, maslahi ya Uingereza na, bila shaka, washirika wetu katika eneo hilo,” ameongeza.

Pamoja na msimamo huo, Starmer alisema Uingereza itaendelea kushiriki katika jitihada za kimataifa za kuhakikisha usalama wa njia muhimu za usafirishaji, ikiwemo Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao ni muhimu kwa biashara ya kimataifa ya mafuta.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa hatua hizo hazimaanishi kujiingiza vitani.

“Tutalinda maslahi yetu na kushirikiana na washirika wetu, lakini hatutaingizwa kwenye vita hii,” amesisitiza.

Kauli hiyo inaonesha msimamo wa tahadhari wa Uingereza huku mvutano ukiendelea kuongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img