23.1 C
New York

Beckham amtolea uvivu Tuchel

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa zamani wa timu ya taifa ya England, David Beckham, amesema haelewi sababu ya kocha Thomas Tuchel kutomuita kikosini beki Trent Alexander-Arnold.

Tuchel ‘amempotezea’ Alexander-Arnold katika kikosi cha wachezaji 35, ambao anajaribu kuangalia watakaomfaa kwenda nao Kombe la Dunia.

Kwa upande wake, Beckham amefananisha uchezaji wa Alexander-Arnold na ule wa Roberto Carlos.
“Ndiyo maana mimi siyo kocha wa England, kwa sababu siwezi kufanya maamuzi kama hayo,” amesema lejendari huyo wa Manchester United.

Aidha, Beckham alimzungumzia pia kile kinachotajwa kuwa ni udhaifu mkubwa wa Alexander-Arnold, kwamba ni mzuri kwenye kuishambulia kuliko kutekeleza majukumu ya ulinzi.

“Hata Roberto Carlos, alikuwa beki bora sana, lakini kwenye ushambuliaji. Sisi ndo tulitakiwa kuziba nafasi yake (kwenye ulinzi) pindi alipokuwa akishambulia,” amesema Beckham.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img