18.5 C
New York

Vita ya Iran yatikisa Serikali ya Trump

Published:

Washington, D.C.

MKUU wa Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi nchini Marekani, Joseph Kent, amejiuzulu wadhifa wake akipinga vikali vita vinavyoendelea dhidi ya Iran, akieleza kuwa havina uhalali wala manufaa kwa taifa hilo.

Katika barua yake ya kujiuzulu aliyomwandikia Rais Donald Trump, Kent amesema hawezi kuunga mkono vita hivyo kwa dhamira njema. “Siwezi kwa dhamira njema kuunga mkono vita vinavyoendelea Iran. Iran haikuwa tishio la haraka kwa taifa letu,”ameandika.

Kent amedai kuwa uamuzi wa kuingia vitani umetokana na shinikizo kutoka Israel pamoja na ushawishi wa makundi yenye nguvu nchini Marekani. “Ni wazi kuwa tulianzisha vita hivi kutokana na shinikizo kutoka Israel na ushawishi wa makundi yenye nguvu ya Marekani,” ameongeza.

Ameonya kuwa hatua hiyo inaweza kuirudisha Marekani katika makosa ya kihistoria kama yale ya vita vya Iraq. “Hii ni mbinu ile ile iliyotumika kutuingiza kwenye vita vya Iraq vilivyosababisha vifo vya maelfu ya wananchi wetu. Hatupaswi kurudia kosa hili,” amesema.

Aidha, Kent amesema haoni sababu ya kuwatuma vijana kupigana katika vita visivyo na manufaa. “Siwezi kuunga mkono kuwatuma vijana wetu kupigana na kufa katika vita ambavyo havina faida kwa Wamarekani,” amesisitiza.

Amehitimisha kwa kumtaka Rais Trump kutafakari upya mwelekeo wa vita hivyo. “Unaweza kubadilisha mwelekeo na kuweka njia mpya kwa taifa letu au kutuacha tuendelee kuelekea kwenye machafuko. Uamuzi uko mikononi mwako,”amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img