TEL AVIV, Israel
SERIKALI ya Israel imeweka wazi kuwa itamshambulia kijeshi, ikiwamo kumuua, kiongozi yeyote atakayeingia madarakani kuiongoza Iran.
Ujumbe huo wa tishio unalenga kiongozi atakayechukua nafasi ya Ayatollah Ali Khamenei aliyeuawa na vikosi vya Israel kwa kushirikiana na Marekani.
Katika taarifa yake, Wizara ya Ulinzi ya Israel imesema hakuna kiongozi wa Iran atakayechaguliwa na utawala wa sasa atakayebaki salama.
“Kiongozi yeyote wa utawala wa kigaidi wa Iran atakayeingia madarakani kuharibu mipango ya Israel, kuitisha Marekani na kukandamiza watu wa Iran hatasalimika,” inaeleza taarifa ya Israel.
Wakati huo huo, taarifa hiyo imesema Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameviagiza vikosi vya jeshi la nchi yake kujipanga kwa lolote litakalofanywa na Iran.
Kwa upande mwingine, Marekani imetangaza kushambulia maeneo takribani 2,000 nchini Iran, ikiwa ni pamoja na kushambulia meli za kivita 17 za Taifa hilo la Kiarabu.


