13.5 C
New York

Man City wapishana na Mbappe

Published:

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Kylian Mbappe, huenda asicheze dhidi ya Manchester City katika mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Timu hizo zitakwaana Machi 11, 2026 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA).

Mbappe hakucheza wakati Madrid ilipokwaana na Benfica katika mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa kutokana na majeraha ya goti.

Kwa mujibu wa ripoti, Mfaransa huyo atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu akiuguza majeraha hayo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, amekuwa na mchango mkubwa kwa Madrid msimu huu.

Katika mechi 33 za michuano mbalimbali alizoshuka dimbani, ameingia kambani mara 38 na kutoa asisti sita.

Kwa Ligi ya Mabingwa, amefunga mabao 10, hivyo kukosekana kwake kunaweza kuwa habari njema kwa safu ya ulinzi ya Man City.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img