6.5 C
New York

‘Nyuma ya ushirikiana’, Chief Godlove ni kitabu kizuri kukisoma

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KWA wapenzi wa mitandao ya kijamii, hasa ‘walevi’ wa habari za burudani, Chief Godlove si jina geni masikioni na machoni mwao.

Ni kijana aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana na ‘staili’ ya maisha ya anasa anayoyaanika mitandaoni. Magari ya kifahari, nyumba kali, mavazi ya gharama, kwa kutaja kwa uchache tu.

Ukweli ulio wazi ni kwamba utajiri wake umekuwa gumzo na wakati mwingine kuibua ‘komenti’ za kutilia shaka chanzo chake.

Kwa zaidi ya asilimia 90, takwimu zinazotokana na maoni (komenti) za habari zinazomuhusu Chief Godlove zimekuwa zikihusisha ukwasi wake na imani za kishirikina.

Hata hivyo, tunaweza kukubaliana kuwa hakuna mwenye ushahidi juu ya hilo, hivyo bado zinapazwa kuitwa ‘dhana zisizo na mashiko’ hadi pale zitakapothibitishwa.

Kwa maana hiyo, itabaki hivi; Chief Godlove ni nembo ya kijana wa kisasa, ‘aliyetoboa’, na ambaye anataka jamii ifahamu kuwa kwake pesa siyo shida zake.

Kwamba, licha ya wengine kumtafsiri kuwa ni mtu anayejikweza, Chief Godlove anaviamsha na kuvipa moto vichwa vya vijana.

Kisaikolojia, anachofanya ni kuziamsha akili za vijana wenzake. Anawafanya waone ni jambo linalowezekana kwa kijana kufanikiwa.

Ndiyo, kama Chief Godlove, ambaye ana umri kama wako, anaishi vizuri, kwanini kwako isiwezekane? Hakuna kinachoshindikana!

Haijalishi Chief Godlove anapitia njia zipi, ujumbe wake kwa kijana ni kwamba mapambano ya kufukuzia maisha mazuri yanapaswa kuwa kipaumbele kila iitwayo leo.

Ujumbe mkubwa anaoupeleka vichwani mwa vijana ni kwamba kufanikiwa katika umri mdogo kama wake ni jambo linalowezekana.

Mara zote katika mahojiano yake, Chief Godlove amekuwa akisisitiza ‘kupambana’ na kuvuja jasho jingi katika kuyaendea mafanikio, bila kujali aina ya kazi unayofanya.

Kwamba haijalishi familia unayotoka ni ya hali ya chini kiasi gani, jitihada zinaweza kukutoa hapo uliopo na kukupeleka katika kilele cha mlima wa mafanikio.

Kuthibitisha hilo, leo hii Chief Godlove ni tajiri, kama anavyoonekana mitandaoni, licha ya kwamba amekuwa akisimulia maisha ya ‘kuungaunga’ aliyoyakuta katika familia yake.

Kwa Chief Godlove, kama si njia aliyotumia kupata mafanikio, basi vijana wanapata somo kwamba kufanikiwa ni zaidi ya historia ya familia unayotokea.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img