6.4 C
New York

Viwanja vya soka vikubwa zaidi duniani

Published:

LONDON, Uingereza

UKIWA na uwezo wa kupokea mashabiki 132,000, Uwanja wa Narendra Modi ndiyo mkubwa zaidi katika ulimwengu wa mchezo wa soka. Uwanja huo uko India.

Nafasi ya pili ni ya Uwanja wa Rungrado Mei Mosi ulioko mjini Pyongyang, Korea ya Kaskazini. Dimba hilo lina uwezo wa kupokea mashabiki 114,000.

Mbali ya soka, Uwanja huo umekuwa ukitumiwa kwa shughuli zingine mbalimbali, zikiwamo za matamasha makubwa ya muziki.

Uwanja wa Michigan, maarufu pia kwa jina la ‘The Big House’ unashika nafasi ya tatu. Ni Uwanja unapatikana Marekani ukiwa unaingiza mashabiki 107,601.

Nafasi ya nne ni ya Uwanja wa Beaver, ambao pia uko Marekani katika Mji wa Pennsylvania. Unapokea mashabiki 106,572.

Unaofuata katika nafasi ya tano ni Uwanja wa Ohio, pia ukifahamika kwa jina la ‘The Horseshoe’. Nao uko Marekani na unapokea mashabiki 102,780.

Katika nafasi ya sita, ni Uwanja wa Kyle Field ulioko Texas, Marekani. Uwanja huo unapokea mashabiki 102,733.

Aidha, Uwanja wa Neyland ulioko mjini Tennessee, Marekani, uko nafasi ya saba ukiwa unaingiza mashabiki 102,455.

Pia, kuna Uwanja wa Tiger unaopatikana mjini  Louisiana, Marekani, ambao kwa sasa unapokea mashabiki 102,321.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img